Serikali Yaunda Kikosi Maalam Cha Kupambana na Fisi Waliokithiri Shinyanga


Kutokana na kukithiri kwa matukio ya Fisi kushambulia wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga hususan watoto, Serikali imeunda kikosi maalumu kwa ajili ya kufuatilia na kuwasaka fisi hao

Kwa miezi 6 sasa, kumekuwepo na matukio ya Fisi kuwashambulia watu katika Manispaa hiyo huku ikiripotiwa watoto wasiopungua 4 kufariki baada ya kushambuliwa na fisi

Kiongozi wa kikosi hicho, Ezra Manjerenga amesema operesheni hiyo inaendeshwa kwa ushirikiano na Wataalamu wa Maliasili Kitengo cha Wanyamapori, Polisi, Viongozi wa vijiji na Sungusungu

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, operesheni hiyo imeanza leo saa 12 alfajiri kwa kufanya msako katika vichaka na mapori yote yaliyopo katika Kijiji cha Nhelegani kwenye vitongoji vya Itogwanh’olo na Ibanza

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad