Shujaa wa 'Hotel Rwanda' akamatwa kwa tuhuma za ugaidi



Mwanamume ambaye jukumu lake la kuwaokoa Wanyarwanda dhidi ya mauaji ya kimbari liliangaziwa katika filamu ya Hotel Rwanda,amekamatwa kwa tuhuma za ugaidi.


Paul Rusesabagina amekamatwa ughaibuni ambako alikuwa anaishi mafichoni.


Shirika la upelelezi la Rwanda linasema alikamatwa kupitia waranti ya kimataifa kwa kuunda na kuongoza "vuguvugu la kigaidi" linaloendesha shughuli zake katika eneo hilo.


Bw. Rusesabagina, 66, alitunukiwa medali ya Rais wa Marekani ya Uhuru 2005, miongoni mwa tuzo zingine za haki za binadamu.


Hajatoa tamko lolote kuhusu tuhuma za sasa dhidi yake lakini amekuwa mkosoaji wa serikali ya Rwanda.


2011, alituhumiwa kuwafadhili wajumu wa serikali ya Rwanda, lakini hakufunguliwa mashitaka yoyote.


Wakati huo, Bw. Rusesabagina alipinga tuhuma dhidi yake na kudai ilikuwa njama ya kumharibia sifa.


Mwaka 2004 filamu ya Hotel Rwanda iliangazia jinsi Bw. Rusesabagina, Mhutu wa aliyemuoa mwenye Tutsi, alivyotumia ushawishi wake - na rushwa- kuwashinikiza maafisa wa kijeshi kumpatia njia salama ya kuwatorosha karibu watu 1,200 kutafuta makazi katika Hoteli ya Mille Collines mjini Kigali.


Kundi la manusura wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Ibuka liliwahi kusema kuwa alitilia chumvi jukumu lake la kuwasaidia wakimbizi kujificha hotelini hapo siku 100-ya mauaji ya kikatili mwaka 1994.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad