Shutuma Dhidi ya TIK TOK, Instagram Yaja na Mbadala wa TIK TOK
0
August 10, 2020
Huku uelekeo wa TikTok ukiwa bado haujafahamika, Instagram inatarajia kuchukua baadhi ya mashabiki wa ‘App’ hiyo kupitia ‘App’ yake iitwayo Reels, inayozinduliwa leo katika nchi takriban 50 zikiwemo Uingereza, Marekani, Japan na Australia
Kama ilivyo TikTok, Reels inawezesha wadau kutengeneza video fupi na kusambaza kwa wadau wengine na wafuasi wako. Reels inawezesha watu kutengeneza video zenye urefu wa hadi sekunde 15 na kuweza kuongeza muziki maarufu
Kwa wanaotarajia kutumia Instagram Reels kupata wafuasi, Instagram imebadili sehemu yake ya ‘Explore’ na kuweka sehemu hiyo kuwa ya Reels na watu wanaweza kuperuzi kama ilivyo kwa TikTok kupitia “For You Page”
Katika 'App' hiyo kuna uwezo wa kuiseti iwe na ufaragha au kuacha ili kila mtu aweze kuipata akitafuta. Kwa wanaotaka kushirikisha marafiki, wakiwa katika hali ya ufaragha wataposti tu kwenye ‘Feed and Stories’ zao binafsi
Tags