Sikiliza Hapa Wimbo wa Kwanza Baada ya Mzee Yusuph Kutangaza Kurudi Kwenye Mziki

 Siku chache baada ya kutangaza kurudi kwenye muziki, Msanii wa taarabu @mzeeyussuf tayari amechia wimbo wake wa kwanza wikiendi hii uitwao, "Najiripua"
-
Hii ni baada ya kuwa nje ya tasnia hiyo kwa takribani miaka minne ambapo mwaka 2016 alitangaza kuacha kuimba taarabu na kujikita katika shughuli za ualimu wa dini na kutoa dawa (mawaidha kwa waumini wa dini ya Kiislamu)
-
Itakumbukwa, Machi 12 mwaka huu @mzeeyussuf kwenye ukurasa wake wa #Instagram, aliandika kuwa anarudi mjini na ataimba mpaka agalegale na wiki iliyopita alipohojiwa na #WasafiFm alifunguka kuwa anarudi rasmi kwenye muziki.


#MzeeYussuf anafanya hivyo akiwa katika maandalizi ya onyesho lake lililokuwa lifanyike kwenye sikukuu ya Eid lakini lilisogezwa mbele kutokana na msiba wa Rais Mstaafu awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ambalo sasa linatarajiwa kufanyika mkesha wa kuamkia sikukuu ya nanenane.

Hii inahitimisha safari yake ya kurudi kwenye muziki, kwa kuachia wimbo wa kwanza tangu alipoacha kuimba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad