Simba Washtuka, Wabadili Siku Ya Kumtambulisha Morrison



UONGOZI wa Simba ni kama umeshtukia kitu, ni baada ya kuchukua maamuzi ya kusogeza mbele siku ya kumtambulisha kiungo mshambuliaji Mghana, Bernard Morrison.


Mghana huyo jana zilizagaa tetesi za kutambulishwa na uongozi wa Simba baada ya kufikia muafaka mzuri na kusaini mkataba wa miaka miwili ya kukipiga Msimbazi.


Kiungo huyo alijiondoa kwenye kikosi cha Yanga mara baada ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la FA iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam iliyomalizika kwa Simba kushinda mabao 4-1.


Taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, kiungo huyo tayari amesaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh 230Mil kwa siri kwa ajili ya kuichezea timu hiyo.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa Mghana huyo atatambuLishWa rasmi Simba Day ambayo imepangwa kufanyika Agosti 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa baada ya kupata ruhusa kutoka TFF.

Aliongeza kuwa mabosi wa Simba wana uhakika mkubwa wa kumpata kiungo huyo mwenye mbwembwe nyingi ikiwemo ya kuupanda mpira kwa juu baada ya kupenyezewa taarifa kutoka kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF inayosimamia kesi yake.

“Simba walikuwa kwenye mipango ya kumtambulisha leo (jana) Morrison, hivyo wamesogeza mbele wakisubiria hukumu yake kutoka kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF ambako kesi yake ipo huko.“Kesi hiyo inamuhusu Morrison na Yanga kwa kila mmoja kumtuhumu mwenzake kufanya makosa kwenye mkataba wake, hivyo siku yoyote itatoa hukumu hiyo TFF.

“Hivyo, utambulisho wa Morrison umepangwa kufanyika Agosti 22, mwaka huu katika siku yao maalum ya utambuLisho wa wachezaji na jezi mpya ya Simba Day,” alisema mtoa taarifa huyo.Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, anayesimamia usajili wa wachezaji wapya alisema: “Inashangaza kwa kuwa bado Morrison ana mkataba na kesi yake bado inasikilizwa, hivyo itakuwa ni ajabu kutangazwa leo (jana) najua kamati inafuatilia mambo yaliyopo.

“Kwa harakaharaka nimegundua kwamba mchezaji ni wetu, nikiangalia naona picha mbaya sana kama mchezaji atasaini na amekuwa na matatizo ya nidhamu kwa muda mrefu, amekuwa akisema kwamba viongozi wa Simba wamekuwa wakimlaghai ili kumpa mkataba.

“Kwa kuwa sisi tumemleta hapa nchini na kumpa mkataba hivyo kila kitu kitajulikana na wao watakuwa wanahusika katika yote kwani ninaiheshimu Simba katika masuala mazima ya uendeshaji na hii kesi ipo kwenye kamati.”

stori: Wilbert Molandi na Lunyamadzo Mlyuka
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad