Tabia 10 za Kuepuka Kuinusuru Figo yako


Figo ni miongoni mwa viungo muhimu vya mwili kwa binadamu kukosa kufanya kwake kazi kunaweza kusababisha magonjwa mazito na hata mauti.

Figo mwilini husaidia kutoa mkojo na uchafu wenye sumu na maji zaidi kutoka mwilini Mkojo unaotengenezwa katika figo hupitia kwenye mrija uitwao” ureta, na huteremka hadi kwenye kibofu na mwisho hutoka kupitia mrija wa urethra.

Leo nimekuandalia mambo 10 yanayoweza kuathiri utendaji kazi wa figo yako.

Utumiaji vidonge vya kupunguza maumivu mara kwa mara
Kubana mkojo kwa muda mrefu
Mwili kukosa maji ya kutosha
Kunywa pombe kali
Kutumia kiwango kikubwa cha chumvi
Kutumia kiwango kikubwa cha sukari
Kutopata muda wa kutosha kulala usingizi
Kula kiwango kingi cha protini
kuvuta sigara
Kunywa chai ya kahawa kupitiliza
Mfululizo wa kufanya mambo haya juu huleta madhara makubwa kwa figo, kikawaida magonjwa ya Figo yamegawanyika katika makundi mawili, kundi la kwanza ni magonjwa ya figo yanayohitaji matibabu ya kawaida na kundi la pili ni magonjwa ya figo yanayohitaji upasuaji.

Magonjwa yanayoweza kutibika ni kama Hitilafu kali ya figo, Ugonjwa sugu wa figo, Maambukizi ya mfumo wa mkojo, Hitilafu za uvimbe (nephritic syndrome).

Na magonjwa yanayohitaji upasuaji ni kama Ugonjwa wa mawe, Shida za uume, Hitilafu za kuzaliwa nazo za wa mkojo mfumo wa mkojo, Saratan.

Hivyo kuweka figo yako katika hali ya usalama inashauriwa kuepukana na mambo kumi hapo juu ambayo hudhoofisha utendaji kazi wa Figo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad