Hassan Nassor Moyo ambaye ni Mwanasiasa mkongwe na mwasisi wa Mapinduzi Zanzibar amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mkoani Tanga
Mzee Moyo alikuwa mwanachama wa Chama cha Afro Shirazi (ASP) tangu kilipoanzishwa Februari 5, 1957 baadaye Februari 5, 1977 akajiunga na chama cha Mapinduzi akiwa na kadi namba 7.
Aidha Mzee Moyo ndiye alikuwa Mratibu Mkuu wa Maridhiano ya Zanzibar ya Novemba 5, 2009 yaliyowakutanisha Rais Mstaafu wa Zanzibar (awamu ya sita), Dk Aman Abeid Karume na Maaalim Seif Sharif Hamad katika kutafuta mbinu ya kuondoa tofauti iliyokuwepo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010.