Tetesi za soka kimataifa


Mkufunzi Arsenal Mikel Arteta anamtaka mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo raia wa Uholanzi Dennis Bergkamp, 51, kurudi katika klabu hiyo kama naibu wake . (The Sun)
Barcelona itakatiza kandarasi ya mshambuliaji wa Uruguay mwenye umri wa miaka 33 Luis Suarez. (RAC1 via Daily Mail)

Chelsea wanataka kutumia fedha zaidi kuliko walivyotumia katika uhamisho uliopita wa wachezaji baada ya kufanikiwa kupata ithibati ya kuwasajili kiungo wakati wa Bayer Leverkusen Mjerumani Kai Havertz ,21, na mlinzi wa Paris St-Germain raia wa Barzil Thiago Silva, 35. (The Times - subscription only)

Thiago amesema ataamua hatima yake ya baadaye katika kipindi cha saa 24 zijazo. (London Standard)

Mmiliki wa zamani wa Inter Milan Massimo Moratti anaamini klabu yake ya zamani inajaribu kumnunua mshambuliaji wa Barcelona Muargentina Lionel Messi, 33. (AS - in Spanish)

Mkufunzi Arsenal Mikel Arteta anamtaka mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo raia wa Uholanzi Dennis Bergkamp, 51, kurudi katika klabu hiyo kama naibu wake . (The Sun)

Leeds United wanamtaka mshambuliaji wa Argentina Nicolas Gonzalez, 22, amesema mkurugenzi wa michezo wa Stuttgart Sven Mislintat. (Yorkshire Evening Post)

Everton wameafikia mkataba na Napoli kulipa £31.5m ili kumpata kiungo wao wa kati Mbrazil Allan,29. (Daily Express)

Mashambuliaji wa Italia Moise Kean, 20, anakaribia kukamilisha mchakato wa kurudi katika klabu yake ya zamani Juventus kwa mkopo. (Tuttosport via Mirror)

Mlinzi wa Manchester United Victor Lindelof, 26, amepongezwa na polisi wa Uswidi kwa kumkamata mwizi aliyekuwa amemuibia ajuza. (Sky Sports)

Wolves wamepiga hatua katika mazungumzo yao na Arsenal kuhusu mkataba wa miaka minne wa beki wa beki Muingereza Ainsley Maitland-Niles,22. (Sky Sports)

Manchester United wako tayari kumtuma kipa wao Moreno Joel Pereira, 24, mjini Huddersfield kwa Mkopo. (The Sun)

Valencia wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Real Madrid Mhispania Borja Mayoral,23. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mkufunzi wa Aston Villa Dean Smith amesema kuwa amefanya mazungumzo na mkurugenzi mpya wa soka wanayemnyatia Johan Lange. (Birmingham Mail)

Bournemouth wamewafuta kazi karibu maafia wao 10. (Bournemouth Echo)
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad