Tetesi za Usajili, Simba, Yanga, Azam FC na klabu nyingine Ligi Kuu leo Alhamisi



Wakati huu wa dirisha la usajili Bongofive inakuletea tetesi za wachezaji wanao toka klabu moja na kuhamia nyingine na wale waliokamilisha sajili zao.


Timu ya Wananchi, Mabingwa wa Kihistoria Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC imetangaza kumsajili Abdallah Shaibu ‘Ninja’ akiwa amerejea kwa mkataba wa miaka miwili.




Ni kama vile miamba ya soka nchini Simba na Yanga wameamua kuibomoa Coastal Union ya Tanga, ni baada ya kudaiwa Mnyama Simba kumsajili, Ibrahim Ame na Mwamnyeto kusajiliwa na Yanga.


MICHEZO FORUM: MITAMBO INAYOMPA JEURI MGUNDA COASTAL UNION NAMNA ...


Klabu ya Yanga inadaiwa kufanya mazungumzo ya awali na straika wa Namungo, Bigirimana Blaise. Hata hivyo Yanga bado inapambana kupata straika mwingine hatari zaidi


Bigirimana Blaise amefunga jumla ya magoli 11 na pasi za mwisho zilizo changia magoli au asisti tano msimu huu.




Inadaiwa kiungo wa Azam FC, Abubakar Salum ‘Sure Boy’ ameuomba uongozi wa timu hiyo wakubali kumuuza kwenda timu ya Wananchi klabu ya Yanga SC.



Klabu ya Simba imeachana na mipango yake ya kutaka kumsajili beki wa Biashara United, Abdulmajid Mangalo katika dirisha hili la usajili baada ya kumsaini Ibrahim Ame kutoka Coastal Union kwa mkataba wa miaka miwili.




Inadaiwa Yanga itamsajili, Abdulmajid Mangalo kutoka Biashara endapo itashindwana makubaliano ya mkataba mpya na beki mkongwe, Kelvin Yondani.


GADIEL: WACHEZAJI SIMBA TUNADENI KUBWA | Divine Radio FM


Yanga yanuia kumrejesha nyumbani beki wa kushoto, Gadiel Michael endapo ataruhusiwa kuondoka Msimbazi katika dirisha hili la usajili. Gadiel amebakisha mwaka mmoja.

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad