Trump aridhia uteuzi wa Republican kwa kumshambulia Joe Biden



Rais Donald Trump ameridhia rasmi uteuzi wa kuwa mpeperusha bendera ya chama chake cha Republican katika kuwania muhula wake wa pili madarakani.


Hatua hiyo anaipokea huku akigubikwa na mvutano wa ghasia za ubaguzi wa rangi, vurugu nyingine na janga la virusi vya corona.


Yote hayo yanazusha hoja ya je, atashindwa dhidi ya mgombea wa Democratic Joe Biden? Mfanyabiashara huyo wa tasnia ya ardhi ya majengo amezungumza katika hatua ya ufungaji wa  kongamano la chama chake baada ya kuhitimisha muhula wake wa kwanza wa urais wa Marekani. Idadi kubwa ya wajumbe ambao walihuidhuria hotuba yake katika viwanja vya Ikulu ya Marekani, pamoja na wimbi kubwa la janga la virusi vya corona wachache walionekana kuvaa barakao huku wakionekana kujongelea kwa karibu zaidi. Ikadariwa zaidi ya watu 2000 wamehudhuria mkutanop huo.


Katika hotuba yake hiyo amesema yeye ndie rais bora kuwahi kushuhudiwa toka zama za Abraham Lincoln ambae alifanikisha taifa kujiondoa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na kokomesha biashara ya watumwa. Hata hivyo aliendelea kutoa ahadi kama atafanya vizuri zaidi endapo atachaguliwa katika uchaguzi ujao. Alisema amefanya mengi zaidi katika kipindi chake cha miaka minne ikilinganishwa na hasimu wake Joe Biden ambae amekuwepo katika siasa kwa miaka 47.


Wapinzani wa Rais Trump wamekuwa wakimkosoa kwa kusema amekuwa chachu ya vurugu. Pamoja na Marekani kuzongwa kwa hali ya ubaguzi wa rangi, bado pia taifa hilo lipo katika makabiliano ya virusi vya corona au kufungua sghule na biashara katika hali yake ya kawaida. Na kadhia ya kimbunga Laura katika eneo la Huba ya Pwani mapema Alhamis imechangia pia hali kuwa mbaya zaidi katika taifa hilo tajiri duniani, ikiwa si zaidi ya miezi miwili liengie katika uchaguzi wake mkuu.


Pamoja na lawama zote kuhusu namna alivyolishughulikia janga la virusi vya corona amestoa ahadi ya kuliangamiza janga hilo ifikapo mwishioni mwa mwaka huu kwa kutumia chanjo. Amesema zipo jitihada za pamoja na wanasayansi wa Marekani na kwamna kutapatikana chanjo salama na madhubuti.


Muda mfupi kabla ya Rais Trump kutoa hotuba yake, Ikulu ya Marekani White House ilitangaza hatua yake ya kununua mashine 150 zenye uwezo wa kupima kwa kasi virusi vya corona, kwa lengo la kusaidia mchakato wa kufungua shule na biashara nyingine kwa namna salama zaidi. Mpinzani wake mteule wa ugombea urais kwa tiketi ya chama cha demokratic amemtuhumu Trump kwa namna yake dhaifu ya kushughulikia janga la corona ambalo limesababisha vifo vya zaidi ya Wamarekani 180,000

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad