Tunasubiri Suprise ya Rais Magufuli - Alikiba
0
August 06, 2020
Staa wa Bongofleva Alikiba amesema siku ya mchezo wa "Team Kiba Vs Team Samatta" August 8 Uwanja wa Benjamin William Mkapa, kutakuwa na mambo mengi ikiwemo burudani na huenda kukawa na Suprise Rais John Pombe Magufuli kwa sababu amemuomba awepo kwenye mchezo huo.
Alikiba amesema Rais John Pombe Magufuli amewaomba watanzania tuweze kudumisha amani kwa sababu yeye amefanya mengi kilichobakia ni sisi kutimiza na usalama utakuepo siku ya mchezo huo.
"Nilimuomba Rais Magufuli aweze kutusaidia kitu kwa hiyo kuna uwezekano wa kuwa na suprise, msije mkashangaa Rais akaja kwa sababu yeye ni mpenzi wa burudani na anatukubali wote mimi pamoja na Samatta, Pia amempongeza sana Mbwana Samatta tulivyokuwa Dodoma kwa kazi kazi nzuri, hivyo tunasubiria suprise yake na chochote kinaweza kutokea kwenye siku ya mchezo huo" amesema Alikiba
Tags