Ugonjwa usio wa kawaida unaosambazwa na kupe wabainika Uingereza



Watu wameombwa kuwa katika tahadhari kwa ugonjwa usio wa kawaida unaosambaa kwa kuumwa na kupe baada ya kubainika kwa mara ya kwanza Uingereza.



Wizara ya Afya imesema kwamba hatari iliyopo kwa umma ni ya chini lakini ni muhimu wawe waangalifu kuhusu kupe hasa wanapokuwa kwenye maeneo ya bustani msimu wa joto.

Ugonjwa huo unasababishwa na vimelea ambavyo vinaathiri chembe nyekundu za damu.

Mgonjwa wa pili aliyeambukizwa ugonjwa huo ambao ni nadra sana kutokea amegunduliwa.

Ugongwa huo unaosambazwa na kupe unaosababisha ubongo kufura mara nyingi hutokana na maambukizi ya virusi.

Dkt. Katherine Russell kutoka wizara ya afya amesema ugonjwa huo ni nadra sana na hivyo basi uwezekano wa maambukizi ni wa chini mno.

“Kupe hupatikana sana kati ya msimu wa kuchipua na pukutizi, kwahiyo ni muhimu ikiwa raia watachukua tahadhari ya juu ili kuhakikishi hawaumwi na kupe wanapokuwa nje wakijivinjari. Na pia tafuta ushauri wa daktari unapoanza kusikia vibaya baada ya kuumwa na kupe.”

Je unawezaje kuepuka kuumwa na kupe?
Wizara ya Afya inasema unastahili kufuata mwongozo uliotolewa:

Unapotembea fuata njia iliyopo na epuka kutembea kwenye nyasi ndefu
Vaa nguo stahiki kama shati la mikono mirefu na suruale ndefu na miguuni iingizwe ndani ya soksi ili kupe asipate mwanya wa kukuuma kwa urahisi
Pia unaweza kutumia dawa kuzuia kuumwa na kupe
Kuwa na mazoea ya kuangalia mara kwa mara mahali uliopo kuhakikisha hakuna kupe hata unapokuwa nyumbani
Ikiwa utaumwa na kupe, anastahili kuondolewa haraka iwezekanavyo kwa kutumia kifaa chenye ncha
 Wasiliana na wizara ya afya haraka iwezekanavyo unapoanza kuhisi vibaya na pia ukumbuke kuwaarifu wahudumu wa afya kwamba uliumwa na kupe.
Lakini ugonjwa huo ni nadra kiwango gani?
Wizara ya afya imesema kwamba imepima mamia ya kupe katika eneo la Devon karibu na anapoishi mgonjwa wa kwanza aliyebainika na ugonjwa huo, lakini wote hawakupatikana nao.

Na pia vipimo vya damu kutoka kwa kulungu kutoka Hampshire katika maeneo karibu na anapoishi mgonjwa mwingine vimeonekana kuwa salama.

Wagonjwa wote wanapata matibabu hospitalini.

Kulingana na Kituo cha Kuzuia Magonjwa Ulaya kimesema ugonjwa huo unasambazwa tu na kupe ambao hupata maambukizi kwa kuumwa na ngombe walio na maambukizi, mbawala na panya buku.

Kuna watu 39 waliothibitishwa kupata maambukizi barani Ulaya. Nje ya Ulaya, ugonjwa huo mara nyingi hutokea tu Marekani.

Je dalili zake ni zipi?

Watu wengi wenye ugonjwa huo ama hawatakuwa wanaonesha dalili au dalili za maambukizi ni za wastani. Hata hivyo, watu wenye mfumo wa kinga ya mwili dhaifu wanaweza kuumwa sana, wakilalamikia dalili za kama mafua, homa, kuhisi baridi, kuumwa na misuli, uchovu na homa ya nyongo ya njano.

Karibia theluthi mbili ya watu wenye maambukizi ya ugonjwa huo hawataonesha dalili. Kwa walio na mafua na homa, kuumwa kichwa na uchovu wanaweza kupata ugonjwa wa utando wa ubongo au kufura kwa ubongo na kupooza mwili.

Shingo inapokakamaa na kuumwa kichwa
Kupata maumivu kwa kuangalia mwanga wa taa
Kuzimia
Kuwa na mabadiliko ya tabia- kama kuchanganyikiwa ghafla
Kuhisi baadhi ya sehemu za mwili zinashidwa kusongea.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad