Mwanaharakati na mwanahabari Maria Sarungi ametoa ushauri kwa vyama vya siasa mbadala kuhakikisha vinatumia vifaa vyao vya mawasiliano (Simu) kama sehemu ya kupasha habari umma bila kulalamika juu ya vyombo vya habari.
Sarungi ametoa ushauri huo leo Agosti 10, 2020 kwenye ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa twitter na kudai kuwa kila mtu anaweza kuwa mwanabahari akitumia simu yake vizuri.
“Ushauri wa bure vyama mbadala na wapenda mabadiliko Acheni kulalamika kuhusu vyombo vya habari! Kila mmoja wetu ana uwezo wa kuwa mwanahabari na mpiga picha kwa sasa! Tumia simu yako na Kuwa Shahidi Picha hizi zimetoka kwenu sisi ni mashahidi! Tuweke record” ameandika Sarungi.
Ushauri wa bure vyama mbadala na wapenda mabadiliko:
— Maria Sarungi Tsehai (@MariaSTsehai) August 9, 2020
Acheni kulalamika kuhusu vyombo vya habari! Kila mmoja wetu ana uwezo wa kuwa mwanahabari na mpiga picha kwa sasa! Tumia simu yako na #KuwaShahidi
Picha hizi zimetoka kwenu 👇🏽sisi ni mashahidi! Tuweke record#TutaelewanaTu pic.twitter.com/6EzTu2c39f
Sarungi ametoa ujumbe huo ikiwa ni saa chache baada ya mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) kutoa muongozo kwa vyombo vya habari juu ya urushaji matangazo.