UMEWAHI Kujiuliza Nini Lengo La Mfuko Mdogo Mbele Ya Suruali Yako Ya Jeans?

Je unaujua mfuko mdogo katika suruali yako ya Jeans? Ndiyo, ule ambao umeshonwa juu kidogo ya mfuko mkubwa wa kulia.

Umewahi hata mara moja kusimama na kujitafakari kwa nini huo mfuko mdogo mbele ya suruali yako ya jeans upo hapo ulipo na nini hasa lengo la mfuko huo zaidi ya pengine kudumbukiza sarafu au jojo ambayo unataka kuja kuitafuna baadae au kuwaza kama ni fasheni tu katika nguo?

Kama hujawahi kujiuliza hilo swali na bado hujui chanzo na lengo la mfuko huo mdogo mbele ya suruali yako ya Jeans usijali kwani  tovuti hii itakueleza chanzo na lengo la mfuko huo.

Mfuko huu ulikuwa unatekeleza jukumu muhimu sana miaka ya nyuma na ndio sababu kubwa iliyopelekea watengenezaji wa suruali za Jeans kuweka mfuko huo juu kidogo ya mfuko wa mbele wa suruali.

“Ni mfuko maalum wa kuhifadhi saa. Ndiyo, inasemekana miaka ya nyuma ya 1,800, watu wengi walikuwa wanapenda kuvaa saa zao katika cheni na kuzifungia katika viuno vyao. Ili kuweza kuweka salama saa zao zisivunjike na kuharibika, Levi, watengenezaji wa kwanza kutengeneza suruali za Jeans wakaamua kuweka mfuko huo mdogo mahali ambapo watu hao wangeweza kuhifadhi saa zao salama na kwa wepesi zaidi.

Hivyo ulianza kama mfuko wa kuhifadhi salama saa za mifukoni, japo baadae ukaanza kupata matumizi mengine kama kuhifadhia sarafu, tiketi za safari, kondomu, na viberiti hasa kwa watumia sigara.

Tangu hapo suruali za Jeans za aina zote zimekuwa zikitengezwa na mfuko huo mdogo bila kujali fasheni iliyopo kwa wakati huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad