Umoja wa Mataifa wakataa pendekezo la Marekani dhidi ya Iran



Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amekataa pendekezo la Marekani la kutaka kurejeshwa vikwazo vyote vya Umoja huo kwa Iran, uamuzi ambao Washington imesema unalenga kuunga mkono ´Magaidi.´ 


Balozi wa Indonesia kwenye Umoja wa Mataifa, ambaye nchi yake ndiyo mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama, amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya wajumbe walio wengi kupinga juhudi hiyo ya Marekani dhidi ya Iran. 


Mataifa mengine wanachama wa Baraza la Usalama isipokuwa Jamhuri ya Dominica yamesema pendekezo la Marekani ni kinyume na sheria kwa sababu nchi hiyo ilijitoa kwenye mkataba wa nyuklia na Iran mwaka 2018. 


Alhamisi iliyopita waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo alisema pendekezo la nchi yake lina msingi wa kisheria licha ya Marekani kujitoa kwenye mkataba wa nyuklia kati ya Iran na madola sita yenye nguvu. 



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad