Unaambiwa Wanasayansi Wangundua SAYARI Mpya Isiyopaswa Kuwepo Angani...
0
February 04, 2022
Wataalam wa anga wamegundua sayari kubwa ambayo wanasema, haipaswi kuwepo, kulingana na nadharia za sasa.
Ulimwengu huo unaofanana na sayari ya Jupita ni mkubwa sana ikilinganishwa na nyota yake mwenyeji, hatua inayokinzana na wazo kuhusu jinsi sayari zinavyoundwa.
Nyota hiyo ilio umbali wa kilomita trilioni 284 , ni ya aina nyekundu na ndogo - ambayo ni aina ya kawaida katika galaxy yetu.
Kundi la kimataifa la wataalam wa angani limeripoti matokeo yake katika jarifda la sayansi duniani.
''Inafurahisha kwa sababu tumejiuliza kwa muda mrefu kama iwapo sayari kubwa kama Jupita na Saturn zinaweza kunda nyota ndogo kama hizo," alisema Profesa Peter Wheatley, wa Chuo Kikuu cha Warwick, Uingereza, ambaye hakuhusika na utafiti wa hivi karibuni
"Nadhani maoni ya jumla yalikuwa kwamba sayari hizi hazikuwepo, lakini hatungeweza kuwa na uhakika kwa sababu nyota ndogo ni dhaifu, Swala ambalo linafanya kuwa vigumu kuzifanyia utafiti , hata ingawa zipo kawaida sana kuliko nyota kama vile Jua, "aliambia BBC News.
Watafiti walitumia darubini nchini Uhispania na Marekani kufuatilia kasi ya mvuto wa nyota ambayo inaweza kusababishwa na sayari zinazoizunguka.
Nyota hiyo nyekundi ilio fupi ina uzani mzito kuliko sayari yake inayoizunguka - kwa jina GJ 3512b. Lakini tofauti yao ya ukubwa ni ndogo mno zaidi ya ilivyo kati ya Jua na Jupita.
Nyota ilio mbali ina ukubwa ambao, ni mara 270 kwa ukubwa zaidi ya sayari.
Kwa kulinganisha, Jua lina ukubwa wa takriba mara 1,050 kuliko Jupita.
Wanaanga hutumia kompyuta kuelezea nadharia zao za jinsi sayari huundwa kutoka kwa mawingu, au "diski", za gesi na vumbi zinavyozunguka nyota ndogo.
Kompyuta hizi zinatabiri kwamba sayari nyingi ndogo zinapaswa kukusanyika karibu na nyota ndogo aina ya M.
"Karibu na nyota kama hizo kunapaswa kuwa na sayari zenye ukubwa wa dunian Dunia au ulimwengu mwingine mkubwa zaidi," alisema mwandishi mwenza Christoph Mordasini, profesa katika Chuo Kikuu cha Bern, Uswizi.
Mfano mmoja halisi wa mfumo wa sayari ambao unaambatana na nadharia ni ule unaozunguka nyota inayojulikana kama Trappist-1
Nyota hii, ambayo iko umbali wa kilomita trilioni 369 kutoka kwa Jua, inasimamia mfumo wa sayari saba, zote zilizo na ukubwa sawa na - au kidogo kuliko ule wa Dunia.
"Hata hivyo, GJ 3512b, ni sayari kubwa ikiwa na ukubwa kama nusu ya Jupiter, na kwa hivyo angalau agizo moja kubwa zaidi kuliko sayari zilizotabiriwa na mifano ya nadharia ya nyota ndogo kama hiyo," alisema Prof Mordasini.
Matokeo hayo yanatoa changamoto kwa wazo la utengezaji wa sayari linalojulikana kama kiboreshaji cha msingi.
"Mara kwa mara sisi hufikiria kuhusu sayari kubwa zinazoanza maisha kataika barafu, inayozunguka nje kwenye diski ya gesi inayozunguka nyota hiyo ndogo, na kisha hukua kwa kasi kwa kuvutia gesi ," alisema Prof Wheatley.
Lakini waandishi wanasema kwamba diski zinazozunguka nyota ndogo hazitoi vifaa vya kutosha kwa hili kufanyaka.
Badala yake, wanazingatia uwezekano kwamba sayari iliundwa ghafla wakati sehemu ya diski ilianguka kwa sababu ya nguvu yake yenyewe.''
Waandishi wa jarida la Sayansi wanapendekeza kwamba kuanguka huko kunaweza kutokea wakati diski ya gesi na vumbi ina zaidi ya theluthi moja ya ukubwa ya nyota kubwa chini ya hali hizi, athari ya mvuto wa nyota inakuwa haitoshi kuweka disc kuwa thabiti.
Prof Wheatley aliandika utafiti katika mwaka wa 2017 ambao ulielezea jitu kubwa la gesi liitwalo NGTS-1b, ambayo ilipatikana na darubini zinazoongozwa na Uingereza nchini Chile.
NGTS-1b pia ni kubwa sana ikilinganishwa na ukubwa wa nyota ya mzazi wake - aina nyingine nyekundu ya M- ambayo iko umbai wa miaka mia sita ya mwanga.
Mwandishi mwenza Hubert Klahr kutoka Taasisi ya Max Planck ya Sayansi huko Heidelberg, Ujerumani, alisema: "Mpaka sasa, sayari za pekee ambazo malezi yake yalikuwa yanaendana na ujumuishaji wa disc chache wa sayari za mchanga, na moto
Tags