Ugonjwa wa fangasi (Candidiasis) husababishwa na vimelea vijulikanavyo kwa kitaalamu kama ‘Candida albicans’. Vimelea hivi hushambulia jinsia zote lakini hushambulia zaidi wanawake sababu ya maumbile yao ya sehemu za siri kuwa na unyevunyevu kitu kinachopelekea wao kuathiriwa zaidi kuliko wanaume.
Watu karibu wote tunaishi na vimelea hivi katika miili yetu kwa kiwango kidogo sana. Kinga ya mwili ikisaidiwa na bakteria wazuri wa mwili ndiyo kupambana na vimelea hivi hata unaona huuguwi ila kinga ya mwili ikiyumba kidogo na bakateria wabaya kuongezeka ndipo hapo unapokutana na ugonjwa kamili.
Tatizo la kuwashwa sehemu za siri ni tatizo kwa watu wengi miaka ya sasa na linawapata watu wa jinsia na rika zote yaani watoto, vijana hata wazee.
Fangasi siyo sababu pekee ya kuwashwa sehemu za siri, kuna sababu na magonjwa mengine yanahusika na tatizo hili na kupona au kuondoka kwa sababu hizo ndiyo kupona kwa huo muwasho.
Sababu za muwasho sehemu za siri za mwanaume
Sababu zifuatazo zinaweza kuhusika na muwasho sehemu za siri kwa mwanaume:
Mzio au aleji
Maradhi ya fangasi
Ugonjwa wa upele
Chawa
Maambukizi ya bakteria
Magonjwa ya zinaa
Lishe duni
Baadhi ya dawa kutibu bakteria
Kushuka kwa kinga ya mwili
Kuambukizana toka mtu mmoja hadi mwingine kwa kuchangia nguo au vifaa
Hali ya hewa nayo yaweza kuwa chanzo hasa mazingira yenye joto sana
Sababu hizi ndizo hupelekea muwasho pia sehemu nyingine za mwili.
Dawa za asili zinazotibu fangasi kwa wanaume
Kumbuka kumuona daktari kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote, ni mhimu kuonana na daktari kwa uchunguzi zaidi ikiwemo kubaini chanzo hasa cha fangasi yako.
1. Mafuta ya habbat soda
Maambukizi ya fangasi yanatokea wakati bakteria wanapozidi juu ya ngozi yako na kupelekea kutokea kwa magonjwa mengi ikiwemo miwasho, upele na ukurutu. Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda ni mazuri kwa tiba karibu kwa kila aina ya fangasi kitu kinachopelekea wanasayansi wengi kuamini kuwa habbat soda ni dawa ya asili na mbadala mhimu zaidi kwa kila mtu kuwa nayo nyumbani.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja. Mengine pakaa kama mafuta yako ya kupakaa sehemu yenye muwasho kutwa mara 3 hadi 3
2. Mafuta ya nazi
Siyo sehemu za ndani tu ya mwili zinazofaidika na mafuta haya ya nazi kama yanavyofanya mafuta mengine ya asili, kama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote vinavyoweza kuidhuru ngozi, haya ni mafuta kwa mwili mzima yaani pakaa kwenye ngozi yote usoni, mwilini, kwenye nywele na kwenye kucha.
3. Mu-aloe vera (mshubiri)
Ngozi hupenda sana Vitamini C na E ambazo zote zinapatikana katika aloe vera na kusaidia kuboresha unene wa ngozi na kuiacha katika hali ya umajimaji. Ikiwa utachanganya jeli ya aloe-vera na mafuta ya asili ya nazi utapata krimu nzuri ya kuongezea viinilishe, mafuta mhimu na unyevunyevu katika ngozi.
Jeli ya Aloe Vera hupenyeza katika ngozi kwa haraka mara nne zaidi ya maji ya kawaida na sifa yake ya kulainisha ngozi husaidia ngozi kubaki na unyevunyevu muda wote.
Mhimu: Pamoja na hizi dawa pia unahitaji kitu kitakachoimarisha kinga yako ya mwili kwa ujumla na kwa sababu hii napendekeza utumie ama unga wa majani ya mlonge au mbegu za maboga kila siku wakati ukiendelea na hizi dawa za fangasi.
Pia hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku, jiweke msafi kila mara na usishirikiane na wengine vitu kama taulo na vifaa vingine vya kuogea.
Epuka vyakula vyenye sukari nyingi na hata sukari yenyewe ikibidi utumie asali badala ya sukari kwenye kila unachohitaji sukari. Epuka pia vyakula vya wanga.
Kama una ugonjwa wa kisukari jitibie kwanza kisukari.