Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Interfax, lililoinukuu wizara ya afya, masaa machache baada ya wizara hiyo kutangaza kuanza uzalishaji.
Hata hivyo baadhi ya wanasayansi wanasema ipo hofu kwamba Urusi inaweza ikawa inaweka mbele kile kinachoonekana kama ufahari wa kitaifa kabla ya usalama.
Hata hivyo chanjo hiyo inaelezwa kwamba itazinduliwa kwa matumizi yake mwoshoni mwa mwezi huu.
Ridhaa ya kutumika kwa chanjo hiyo inatolewa kabla ya majaribio ambayo kwa kawaida yanahusisha maelfu ya watu, ijulikanayo kama awamu ya tatu.
Kwa majaribio ya namna hiyo, inatazamwa kama viashira vya awali vya msingi kwa chanjo hiyo kupata idhini ya kesheria kwa matumizi yake.