Urusi Yaanza Kuzalisha Chanjo ya Corona kwa Matumizi ya Umma



Urusi imeanza uzalishaji wa chanjo mpya ya ugonjwa COVID-19.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Interfax, likinukuu wizara ya afya.

Urusi inasema chanjo hiyo iliyogunduliwa na taasisi ya Gamaleya na kuwa ya kwanza kutengenezwa, itazinduliwa mwishoni mwa mwezi huu.

Tarehe 11 mwezi huu Rais Vladmir Putin wa Russia alitangaza kuwa, nchi yake imegundua chanjo ya kwanza kabisa ya virusi vya corona inayotoa kinga ya kudumu dhidi ya virusi hivyo.

Putin alisema kuwa tayari binti yake mmoja amepewa chanjo hiyo inayozuia maambukizi ya virusi vya corona na maradhi ya COVID-19.

Zaidi ya watu 21,385,925 wameambukizwa virusi vya corona kote duniani. Marekani inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya waathirika na watu walioaga dunia kutokana na virusi hivyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad