China, Urusi na Iran ni kati ya nchi zinazotaka kushawishi uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka huu, mkuu wa Idara ya I
Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa Idara hiyo ilisema nchi za kigeni zilikuwa zinatumia ”njia za ushawish” kuyumbisha kura.
Ilisema China haikutaka kuchaguliwa tena kwa Rais Donald Trump huku Urusi nayo ilitaka kumuumiza Joe Biden wa Democrat.
Wakuu wa ujasusi wanaishutumu Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa mwaka 2016.
Wanasema Urusi ilitaka kusaidia kuongezea nguvu kampeni ya Bw Trump,ikiwemo kueneza habari za uongo mtandaoni. Urusi imekana madai hayo.
Alipoulizwa katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa alichopanga kufanya kuhusu ripoti kuhusu kuingilia uchaguzi, Rais Trump alisema utawala wake utaangalia “kwa karibu” suala hilo.
Tangazo hilo linakuja wakati kukiwa na madai ya Bw. Trump kuhusu hatari ya kupigiwa kura ya posta au barua pepe.
Amedai kuwa uchaguzi uahirishwe ili kuzuia ”uchaguzi wa udanganyifu kuwahi kutokea katika historia,” kauli iliyosababisha upinzani hata miongoni mwa wanachama wa chama chake.
Rais Trump wa Republican anasaka ushindi wa awamu ya pili ya miaka minne madarakani. Mpinzani wake ni mpeperusha bendera wa Democratic, Makamu wa Rais wa zamani , Joe Biden.
Taarifa hiyo imesema nini ?
William Evanina, mkuu wa Kituo cha kitaifa cha Usalama na kupambana na ujasusi (NCSC), alitoa taarifa hiyo Ijumaa.
Nchi za kigeni zinajaribu kupendelea matakwa ya wapiga kura, kubadilisha sera za Marekani, “kuongeza mizozo” nchini “na kudhoofisha imani ya watu wa Marekani katika mchakato wetu wa demokrasia”, Bwana Evanina alisema.
Kiongozi huyo amesema hatahivyo, itakuwa vigumu hata hivyo kwa maaduo kuingilia kati na kudhibiti upigaji kura na matokeo,”Donald Trump
Nchi nyingi ”zina upendeleo kuhusu nani ashinde uchaguzi”, alisema, lakini Mkurugenzi huyo wa kupambana na ujasusi amesemema ” awali wanazitazama” China, Urusi na Iran:
China ”inapenda kuona Trump akikikosa kiti hicho ” taarifa hiyo imeeleza na kuongeza kuwa China imekuwa ”ikiongeza jitihada za ushawishi” kabla ya kura.
Urusi inatafuta kupaka matope nafasi anayoiwania bwana Biden huku washirika wenye uhusiano na Urusi ” pia wanatafuta kumpiga jeki Trump kwenye mitandao ya kijamii na televisheni”
Iran inajaribu ” kudhoofisha taasisi za chama cha Democratic Marekani ”, bwana Trump na ”kuigawanya nchi” kwa kusambaza taarifa za uongo na ”maudhui kuipinga Marekani ” mtandaoni. Jitihada zao zinasukumwa na imani kuwa muhula wa pili wa rais ” utasababisha muendelezo wa shinikizo la Marekani juu ya jitihada za kuchochea mabadiliko ya utawala”.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa, Bwana Trump alisema Urusi “inaweza” kuingilia uchaguzi wa mwaka huu, lakini ilitupilia mbali wazo kwamba nchi hiyo inaweza kuwa inajaribu kumsaidia kushinda muhula wa pili. “Ninadhani mtu wa mwisho Urusi inataka kuona ikishinda ni Donald Trump,” alisema, “hakuna mtu ambaye amekuwa mkali kwa Urusi kuliko mimi.”
Pia alisema China “itapenda” ikiwa itashuhudia kaipoteza kiti hicho , akisema kwamba “watamiliki nchi yetu” ikiwa Joe Biden atashinda.
Kutolewa kwa taarifa hiyo kunakuja baada ya wanachama wa chama cha Democratic kueleza wasiwasi wao kuhusu majaribio ya mataifa ya nje kushawishi kura.