UTAFITI: Kuku wa Kienyeji Wanaouzwa Mitaani Wabainika sio wa Kienyeji



Utafiti uliyofanywa na Shirika la Usalama na Ustawi wa Wanyama Duniani (World Animal Protection) umebaini kuku wengi wanaodaiwa kuwa wa Kienyeji katika maeneo mbalimbali nchini si wa kienyeji kama inavyosemwa

Utafiti huo umebaini kuku hao si wa kienyeji bali ni kuku wa kisasa maarufu kama kuku wa kizungu wanaofugwa majumbani kwa kupewa majani pamoja na dawa mbalimbali za kuwakuza na kuwafanya kuwa wagumu

Msemaji Mkuu wa Shirika hilo, Victor Yamo alisema utafiti huo ulifanywa Juni hadi Julai mwaka huu katika Mikoa ya Arusha na Dar es Salaam hivyo watumiaji wanapaswa kuwa makini

Utafiti huo ulifanyika kwa lengo la kujua walaji wananunua nyama za aina gani, kutoka wapi pamoja na kuangalia kama wanafahamu ubora wa chakula na matumizi ya dawa za wanyama    
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad