Utafiti: Wanawake Wawili Kati ya 10 Wana Utapiamlo


Kondoa. Utafiti wabaini kuwa kati ya wanawake 10, wawili wanakabiliwa na utapiamlo hivyo kuwapo hatari ya vifo vinavyotokana na uzazi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa, Msofeni Dakawa ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge alisema hayo katika maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yaliyofanyika Kata ya Kingale wilayani humo.

Alisema utapiamlo unasababishwa na lishe duni kwa wanawake wajawazito na kuchochea hatari ya kujifungua watoto njiti, waliodumaa au kuwaharibika kwa mimba na vifo.

“Bado kunachangamoto zinazomkabili mjamzito na mtoto chini ya miaka mitano, ikiwa ni pamoja na kuchelewa kuhudhuria kiliniki wakati wa ujauzito, kutofika kabisa kiliniki, kujifungulia nyumbani ama kwa wakunga wa jadi ambao hawana usalama,kukosa mahitaji ya msingi Kama vile chakula,muda wa kupumzika,”alisema

Ofisa Lishe Wilaya Dorice Munishi alisema unyonyeshaji ndani ya miezi sita mfululizo unamwezesha mama kutopata hedhi na umbo lake hurudi katika hali nzuri
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad