Ll
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM (UVCCM),Zanzibar umelaani vikali matamko yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vyama vya saisa akiwemo mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad kwa madai kuwa yana viashiria vya uvunjifu wa Amani kuelekea katika uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu.
Akizungumza na Wandishi wa Habari ofisini kwake, Naibu Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM (UVCCM),Mussa Haji Mussa amesema kwamba UVCCM unalaani vikali matamko yanayotolewa na vongozi hao wa vyama vya Siasa yenye viashiria vya uvunjfu wa amani na utulivu uliopo nchini.
Alisema kuwa UVCCM umechshwa na kauli za Maalim Seif Sharifu Hamad na kutoa wito kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na taasisi zinazoshughulikia masuala ya uchaguzi kuchuka hata kali za kisheria kutokana na kauli zake.
"Maalim Seif Sharif Hamad alitoa kauli kama vile 'liwalo na liwe, sasa imetosha, kaeni tayari kwa lolote' ambapo kaul hizo zinakwenda kinyume na matamko ya vyama vya Siasa ambalo limetiwa saini na vyama vyotea kuridhiwa na tume ya uchaguz ZEC," alisema Naibu katibu Mkuu.
Aliongeza kueleza kwamba kwa kipindi ambacho taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu matamko kama hayo yanaaswa kutovumuliwa na watoaji kuchukuliwa hatua ili kulinda Amani iliyopo.
Aidha alitoa wito kwa viongozi wa Din,Vijaa na wananchama wa chama cha mapinduzi kulaani vikali matamshi yanayotolewa na viongozi hao na kuhakikisha wanalinda Aman na umoja uliopo
"UVCCM tunatoa wito kwa viongozi wa Dini, vijana na wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM na Wazanzibar wote kulaani kauli zenye viashiria vya uvunjifu wa Amani na kuhakikisha kuwa tunlinda mani y Nchi yetu kwa gharama yoyote ile," alisema Naibu katibu Mkuu huyo.
Katika hatua nyingine aliwata wananchi na wananchama wa vyama vya Siasa kutokukubali kurubuniwa na kiongozi yoyte badala yake wanapoambiwa jambo wlipime kabla ya kutoa maamzi na kueneza chuki.
"Wananchi wamekuwa wakijazwa maneno na chuki juu ya wagombea ambao wamewekewa pingamizi bila ya kujua kwamba Suala la Pingamz lipo chini ya sheria kwa mujibu wa kanuni za uhaguzi kifungu namba 51 (1) cha sheria y uchaguzi namba 4 ya mwaka 2018, ambapo mgombea yoyote wa chama anaweza kuwekewa pingamizi" alieeza
Hata hivyo alieleza kwamba ili uwe a uchaguzi ulio huru na haki ni pamoja na wagombea wa ngazi zote kuheshimu kanuni na sheria za uchuguzi ikwemo kuwekewa pangamizi ambapo anayo mgombea anayo fursa ya kukata rufaa.
"Ndugu Waandishi wa Hbari,Mtakumbuka hata mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk Magufuli na Prof Lipumba wliwekewa pingamizi na kusikilizwa na badae kubainika halina mantiki lilitupiliwa mbali"alieleza Naibu atibu mkuu huyo.
Mkutano wa Waandishi wa Habari na Naibu katibu Mkuu huyo ulifanyika katika kuu za Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM, UVCCM Maisara Mjini Unguja.