Vigogo CCM Waliokatwa Wamtaja Mungu

Siku chache baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwakata baadhi ya wagombea ubunge wengi wakiwa ni vigogo, wametoa ya moyoni kuhusu uamuzi uliofanywa dhidi yao, huku wakimtaja Mungu.

Wakizungumza mwishoni mwa wiki na mwandishi wetu, wagombea hao ambao baadhi yao walikuwa mawaziri au maofisa wa ngazi ya juu serikalini, wamesema wamekubaliana na uamuzi huo uliofanywa na vikao vya juu vya chama chao jijini Dodoma wiki iliyopita. Baadhi ya wagombea hao ni hawa wafuatao:

CHARLES KITWANGA

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga ambaye pia aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani, alisema aliyeteuliwa na chama hicho, ni uamuzi wa Mungu, hivyo hana sababu ya kupinga uamuzi uliofanywa na vikao vya juu vya CCM.

“Ninampenda mwenyezi Mungu, ninampenda Rais wangu, ninakipenda chama changu,” alipoulizwa kama atashiriki kampeni, alisema atashiriki kama kawaida.

“Mimi ni mtu wa Mungu, siwezi kumkosea Mungu. Akitoka Mungu duniani anakuja rais, hakuna mwingine. Sasa kama nampenda Mungu, nitashindwaje kumpenda rais?” alihoji.

Kitwanga alisema Rais Magufuli ni rafiki yake wa siku nyingi, hivyo

anaamini kila anachokifanya ni kwa nia njema na yeyote atakayezungumza kinyume chake, atakuwa anamkosea Mungu.

PAUL MAKONDA

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam; Paul Makonda, alitumia ukurasa wake wa Instagram kutoa maoni yake kuhusu uteuzi huo, huku naye akimtaja Mungu, aliandika hivi:

“Ninamwabudu Mungu aliye hai hata kama asipojibu sawa na maombi yangu, bado atabaki kuwa Mungu.”

Makonda alipoteza ukuu wa mkoa baada ya kuchukua fomu ya kuomba ubunge na nafasi yake kubaki wazi, hivyo Rais John Pombe Magufuli, kumteua Aboubakar Kunenge kushika nafasi yake. Katika kura za maoni katika jimbo la Kigamboni, Makonda alishika nafasi ya pili akiongozwa na Dk Faustine Ndugulile ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo katika kipindi kilichopita.

Dk HARISSON MWAKYEMBE

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ambaye aliangushwa katika kura za maoni na wajumbe katika Jimbo la Kyela, mkoani Mbeya alisema ameupokea uamuzi wa vikao vya juu vya chama chake cha CCM kwa mikono miwili.

Alipoulizwa kama atashiriki katika kampeni, alisema atashirikiana na wateule kukiwezesha chama kupata ushindi wa kishindo kwa kumtanguliza Mungu.

“Ninayaheshimu maamuzi ya chama, kilichobaki ni kukisaidia ili wateule waweze kupata ushindi wa kishindo, kwa kumtanguliza Mungu,” alisema Dk Mwakyembe ambaye kwenye kinyang’anyiro cha kura za maoni jimboni kwake, alikuwa mshindi wa tatu.

MARY CHITANDA

Mary Chitanda alikuwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Tanga na alikuwa mjumbe wa Seneti bungeni. Alipoulizwa anapokeaje taarifa za kukatwa, alisema:

“Nimepokea vizuri uamuzi wa chama, kwa sababu ni utaratibu wa chama kila unapotokea kipindi cha uchaguzi mkuu, wanachama wanajitokeza wengi kugombea na mwisho anateuliwa mmoja…ndivyo Mungu alivyopanga,” alisema.

ANDREW CHENGE

Aliyekuwa Mbunge wa Bariadi mkoani Simiyu, Andrew Chenge ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwenyekiti wa Bunge na aliongoza katika kura za maoni za wajumbe, alipoulizwa kuhusu uamuzi wa NEC, alijibu kwamba amefurahishwa sana.

“Nimefurahishwa sana ,” alijibu kwa kifupi. Alipoulizwa kama yupo tayari kushiriki katika kampeni zitakazoanza leo Mungu akimjaalia, alitoa jibu lilelile; “Nimefurahishwa sana,” akakata simu.

ADADI RAJABU

Aliyekuwa Mbunge wa Muheza, mkoani Tanga Adadi Rajabu alisema amepokea matokeo ya maamuzi ya vikao vya juu kwa roho moja tu. Aliahidi kushirikiana na kumpigia kampeni mgombea aliyepitishwa na chama hicho kuwania ubunge wa jimbo hilo.

WILLIAM NGELEJA

Aliyewahi kuwa Waziri wa Madini na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, alisema ataendelea kumuunga mkono aliyeteuliwa na amewashukuru wananchi, lengo likiwa ni kukipa ushindi wa kishindo chama chetu,” alisema Ngeleja Aliwashukuru wana Sengerema kwa kumuamini kwa miaka 15 na kuwa mwakilishi wao.

Uteuzi wa hivi karibuni, chama kilimteua Tabasamu Mwagao kupeperusha bendera ya CCM.

FURAHA DOMINIC

Furahia Dominic aliyeongoza kura za maoni katika Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam, alisema amekubaliana na uamuzi wa vikao vya juu vya chama kumteua Askofu Josephat Gwajima kupeperusha bendera zao.

“Namuunga mkono Askofu Gwajima na tutatumia mbinu za vijana kumng’oa Mdee (Halima Mdee) anayewania tena jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).”

Gwajima alishika nafasi ya pili katika kura za maoni, ingawa kateuliwa kulitetea jimbo hilo (Kawe). Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Dk Charles Kitima alisema vyama vyote vya siasa vimeonesha ukomavu wa demokrasia.

“Tuliona kila chama kikifuata mifumo yao ya vyama, wameanzia ngazi ya chini kabisa hadi juu ambapo kila ngazi wajumbe wametoa maoni yao na kufanya mchakato huo kuwa shirikishi kwa vigezo vyote. Hii inadhihirisha demokrasia imo kwenye vyama hivyo,” alisema Dk. Kitima.

Makala; Elvan Stambuli, Uwazi

OPEN IN BROWSER

Global Publishers · Global Publishers · 1 hour ago

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad