Viongozi wa ECOWAS wawasili Mali katika juhudi za usuluhishi



Wapatanishi kutoka jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS wamewasili nchini Mali, kwa mazungumzo yenye azma ya kubatilisha mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini humo mwanzoni mwa wiki hii. 


Ujumbe huo unaoongozwa na rais wa zamani wa Nigeria Goodluck, unatarajiwa kukutana na wanajeshi walioongoza mapinduzi hayo, na pia rais Ibrahim Boubacar Keita aliyewekwa kizuizini. ECOWAS yenye nchi 15 wanachama imechukua msimamo mkali dhidi ya wanajeshi walioiangusha serikali ya rais Keita, kwa kuwafungia mipaka na mtiririko wa fedha. 


Duru za kidiplomasia zinasema ECOWAS inaelewa kuwa kumrejesha madarakani Keita ni mchakato usiowezekana, na badala yake watashinikiza kuundwa kwa serikali ya mpito, ambayo kwa mujibu wa kanuni za jumuiya hiyo, ndio itaisimamia. 


Hayo yakiarifiwa, wanajeshi wanne wa Mali wameuawa katika mripuko a bomu la kutegwa kando ya barabara katika eneo la katikati mwa nchi, na mwingine mmoja amejeruhiwa vibaya katika shambulio hilo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad