Wabunge wa chama cha Christian Kataeb cha Lebanon wajiuzulu ubunge



Katika kadhia nyingine, mke wa balozi wa Uholanzi nchini Lebanon amefariki leo kutokana na majeraha yaliyosababishwa na mlipuko uliotokea kwenye bandari ya Beirut Jumanne iliyopita. Taarifa hiyo imetolewa na wizara ya mambo ya nje ya Uholanzi. 


Wizara hiyo imeelezea masikito juu ya kifo cha mama huyo aliyekuwa na umri wa miaka 55. Syria imesema wananchi wake 43 walikuwa miongoni mwa watu waliokufa kutokana na mlipuko wa mjini Beirut. Wakati huohuo wabunge wa chama cha wakristo cha Kataeb wamejiuzulu ubunge. 


Mwenyekiti wa chama hicho Sami Gemayel amesema wabunge hao wamejiondoa kutoka kwenye bunge hilo la wabunge 128 ili kupigania nchi wanayoitaka isiyobagua baina wa watu wa Lebanon. Gemayel amesema hayo kwenye maziko ya katibu wa chama hicho aliyekufa kutokana na mlipuko wa jumanne iliyopita. Chama cha Kataeb kilikuwa na wabunge watatu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad