Wataalamu wa masuala ya sayansi wanaotafuta maisha nje ya sayari hii, katika anga za juu watahitajika kusubiri zaidi, kwani kuna dalili ya uwepo wa viumbe katika anga za juu wajulikanao kama Aliens.
Mradi wa kutafuta viumbe hao una gharama za zaidi ya dola milioni 100, lakini bado mpaka sasa bado haujapata chochote tangu uzinduliwe,mwaka mmoja uliopita. Shughuli ya kutafuta viumbe hao wa ajabu zinafanywa kwa kutumia darubini kubwa zaidi ambayo inasikiliza dalili yoyote ya kuwepo kwa viumbe aina ya ‘Aliens’ na wengineo.
Darubini hiyo iliyopo West Virginia, Marekani, ni moja ya darubini zenye nguvu zaidi duniani, zenye uwezo wa kutafuta dalili za kuwepo kwa teknolojia ambayo iliundwa na viumbe vilivyo nje ya sayari ya dunia.
Mwaka uliopita mradi huo ulifuatilia nyota lilioenda kwa jina Tabby, ambayo ilikuwa na tabia iliyosababisha watu kufikiri kuwa ilikuwa na viumbe vyenye maisha ndani yake.