Wafanyakazi 16 wa Bandari ya Beirut Wakamatwa


Siku mbili baada ya mripuko mkubwa katika eneo la bandari katika mji mkuu wa Lebanon , Beirut wafanyakazi 16 wa bandari hiyo katika mji huo ulioko katika pwani ya bahari ya Mediterania wamekamatwa.

Kwa mujibu wa mwanasheria mkuu wa jeshi la nchi hiyo Faki Akiki, uchunguzi unafanyika dhidi ya maafisa wa bandari pamoja na wa forodha.

Serikali ya Lebanon , ambayo inakabiliwa na mbinyo mkubwa kutoka kwa umma wa nchi hiyo, wameahidi kutoa maelezo ya haraka kuhusiana na chanzo cha mripuko huo.

Wengi wa wananchi wa nchi hiyo wanataka ufanyike uchunguzi wa kimataifa. Wafanyakazi wa uokozi wanajaribu kuwatafuta watu 100 ambao hawajulikani waliko.

 Idadi ya watu waliofariki kwa mujibu wa wizara ya afya imepanda na kufikia watu 149.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad