Wahitimu wa Kidato cha Sita Wanza Rasmi Kozi JKT.
0
August 04, 2020
Wahitimu wa kidato cha sita wapatao 1,366 wameanza rasmi kozi kwa mujibu wa sheria ya kundi maalumu katika kikosi cha JKT 833 Oljoro mkoani Arusha huku watatu miongoni mwao wakirudishwa nyumbani kutokana na kugundulika wana ujauzito.
Hao ni kati ya wahitimu wa kidato cha sita wapatao 2,689 waliopangiwa mafunzo hayo ya majuma sita katika kambi hiyo ya Jeshi la kujenga taifa, JKT Oljoro iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Akifungua rasmi mafunzo hayo, Mkuu wa Kikosi cha JKT 833 Oljoro Luteni Kanali Joel Meidimi ametaja malengo ya mafunzo hayo na kwa upande mwingine amekemea tabia ya wanafunzi hao kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi ambayo hatma yake upata ujauzito.
Kozi hiyo inatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 25 ya Mwezi Ujao wa Septemba 2020.
Tags