Wataalamu wa masuala ya afya ya umma siku ya Ijumaa walielezea wasiwasi wao kuhusu tukio la mkutano wa chama cha Republican katika ikulu ya White House iliyoongozwa na rais Donald Trump ambapo baadhi ya wageni waalikwa 1500 hawakuvaa barakoa na kusema huenda baadhi ya wageni hao walileta bila kukusudia na kueneza virusi vya corona.
Dkt Leana Wen, daktari wa masuala ya dharura na Profesa wa afya ya umma katika chuo kikuu cha George Washington, amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba kulikuwa na watu waliokuwa na maambukizi ya virusi hivyo lakini hawafahamu hali zao.
Viti vilipangwa umbali wa inchi chache badala ya futi 6 zilizopendekezwa na kuwaacha washirika hao na nafasi ndogo ya kutimiza sharti la kujiweka kando na watu.
Ni wageni waliotarajiwa kuwa karibu na Trump na naibu wa rais Mike Pence ndio waliotarajiwa kupimwa ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi hivyo.