Watalii Waendelea Kumiminika Tanzania, Ndege Kubwa Zatua na Mamia


Sekta ya utalii nchini imeendelea kufunguka kwa kasi ambapo ndege kubwa za kimataifa zimeingia nchini zikiwa na watalii wengi.

Hivi karibuni, ndege ya KLM imetua katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro ukiwa na watalii 177 wenye nia ya kutembelea vivutio mbalimbali nchini.

Ndege ya KLM ilipata heshima ya kumwagiwa maji kwakuwa ilikuwa mara ya kwanza kutua kwenye uwanja huo, Jumanne usiku, tangu usafiri wa kimataifa ulipozuiwa kwa muda miezi minne iliyopita kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira aliwapokea watalii waliokuja na ndege hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Uwanja wa Ndege (KADC), Christina Mwakatobe pia alikuwa na wawakilishi wengine wa kampuni hiyo na Serikali, walioshuhudia ndege hiyo aina ya Boeing 777 ikitua nchini.

Ndege nyingine kubwa zilizotua KIA ni Crystal Cruises, Gulfstream ya Croatia, Dreamliner A7-BCG, RwandAir. Makundi mengine ya watalii yameendelea kuingia kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Tunashukuru tumefanikiwa kupata watalii wengi, kutokana na mkakati uliowekwa na Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli katika kukabiliana na covid-19, kutuondolea hofu na kuchukua tahadhari dhidi ya virusi hivyo,” Mkuu wa Mkoa, Mghwira amesema. 
“Kumiminika kwa watalii nchini kwetu kuna maana kubwa sana kwetu. Dunia itatuelewa kuwa tulichukua uamuzi sahihi katika kupambana na tatizo hili na sasa maisha yanaendelea vizuri, tumeionesha dunia njia sahihi,” ameongeza.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Qatar amesema kuwa kurejea kwa safari za ndege kuingia Tanzania kuna maana kubwa kwao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad