Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso leo Agosti 19, 2020 amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Igunga, Raphael Merumba, na Bodi yake nzima kupisha uchunguzi baada ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo kulalamika kuwa anawafanyia unyanyasaji ikiwemo kuwadai rushwa ya ngono.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Igunga (IGUWASA), Raphael Merumba, na Bodi yake nzima kupisha uchunguzi baada ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo kulalamikia kuwafanyiwa vitendo vya unyanyasaji ikiwemo kuwadai rushwa ya ngono.
Naibu Waziri Aweso amefikia maamuzi hayo akiwa ziara mkoani Tabora na kufanya kikao cha ndani na wafanyakazi wote wa Mamlaka ya Maji Safi mjini Igunga na ndipo walipoanza kumuelezea changamoto wanazokutana nazo ikiwemo Mkurugenzi huyo kuwaomba wafanyakazi wa kike rushwa ya ngono.
Baada ya kusikiliza kero hizo, Aweso akachukua maamuzi haya, “Kwahiyo hapa tumepata maelezo ya Wafanyakazi lakini kwa kipindi hiki Mkurugrenzi, Mwenyekiti na Bodi yako mtupishe kidogo, wakurugenzi wa Mamlaka za Maji msinyanyase wafanyakazi wenu, na kwa yoyote atakayenyanyasa wafanyakazi wake sisi hatutamchekea”, amesema Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.