WHO na Unicef zataka shule zifunguliwe Afrika


Baadhi ya nchi zimewaruhusu wanafunzi wa mwaka wa mwisho kurudi shule ili wafanye mitihaniImage caption: Baadhi ya nchi zimewaruhusu wanafunzi wa mwaka wa mwisho kurudi shule ili wafanye mitihani

Shirika la afya duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa mataifa la watoto- Unicef yameyazitaka serikali za Afrika kufungua shule zenye mazingira salama wakati huu wa janga la corona.

Wanasema kufungwa kwa shule kwa muda mrefu kuna madhara kwa wanafunzi na mashirika hayo yanazitaka serikali kuwekeza katika huduma za usafi ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona katika taasisi za masomo.

Mashirika hayo mawili yamesema kuwa wanafunzi wanawekwa katika hatari ya lishe duni, mimba za utotoni na ghasia wakati huu wa kurefushwa kwa muda wa kukaa nyumbani.

Shule katika bara la Afrika ni "mahala salama " kwa watoto, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa WHO Matshidiso Moeti.

"Hatupaswi kusahau juhudi zetu za kudhibiti Covid-19. Wakati nchi zinafungua shughuli za kila siku kwa kuzingatia usalama, tunaweza kufungua tena shule ," alisema katika mkutano wa video Alhamisi.

Kufungwa kwa muda mrefu kwa shule kunaathiri maisha ya baadae ya watoto na jamii, kwa mujibu wa Mkurugenzi mkuu wa Unicef wa kikanda Mohamed Fall.

Ni nchi sita tu za Afrika ambazo zimefungua kikamilifu shule, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika nchi 39 na WHO na Unicef.

Baadhi ya nchi zilifunguliwa na baadae kufungwa kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.


Nyingine zinafungua shule kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa masomo yao kwa ajili ya kufanya mitihani muhimu.



Nchi kama Kenya zimefuta mwaka wa masomo wa 2020.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad