WHO yazitaka nchi za Afrika kufungua shule kukwepa mimba kwa wanafunzi


Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto (UNICEF) yamezihimiza nchi za Afrika kufungua shule na kuhakikisha watoto wanakuwa salama dhidi ya virusi vya corona.

Mashirika hayo yamesema kuendelea kufunga shule kwa muda mrefu  kunahatarisha ustawi wa watoto hao ikiwa ni pamoja na kutopata mlo kamili,  mimba za utotoni pamoja na aina mbalimbali za uhalifu.

“Lazima tukahikishe kuwa juhudi za kudhibiti virusi vya corona hazitufanyi  tuishie kuwa na kikazi kibovu. Kama mbavyo nchi zinafungua biashara kwa  usalama, pia tunaweza kufungua shule” Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO Afrika. 

Nchi sita pekee kati ya nchi 39 za Afrika ndizo zilizofungua shule kwa mujibu wa takwimu za WHO na UNICEF, baadhi ya nchi hufungua shule kisha kuzifunga  baada ya maambukizi ya corona kuanza kuongezeka, huku nyingine zikifungua  kwa ajili ya wanafunzi wanaomaliza au wenye mitihani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad