Yanga Yazindua Rasmi Wiki Ya Wananchi Dodoma


KLABU ya Yanga, imeanza sherehe zao kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo jana Jumamosi uzinduzi ulifanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa klabu hiyo na wanachama wao.



Katika uzinduzi huo, yalifanyika maandamano ya amani kuanzia Uwanja wa Jamhuri na kumalizikia Viwanja vya Mashujaa jijini humo.Lengo la maandamano hayo ni kuwa karibu na wananchi pamoja na kusaidia jamii katika uchangiaji wa damu.



Zoezi la kuchangia damu lilifanyika katika Viwanja vya Mashujaa likiongozwa na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msola, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa, Suma Mwaitenda, Ofi sa Mhamasishaji, Antonio Nugaz na wengineo.



Kilele cha Wiki ya Mwananchi inatarajiwa kuwa Agosti 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar ambapo Yanga itacheza mechi ya kirafi ki dhidi ya Aigle Noir C.S ya Burundi.Katika kilele hicho, Yanga itatambulisha kikosi chake cha msimu wa 2020/21, benchi la ufundi pamoja na jezi zao.



Katika hatua nyingine, Yanga inatarajiwa kupambana na Coastal Union katika mchezo maalum wa Kombe la GSM utakaochezwa Agosti 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.



Katibu Mkuu wa Coastal Union, Rashid Mgweno, alisema: “Mchezo huu wa GSM Cup umetokana na makubaliano ya mauzo ya mchezaji, Bakari Nondo Mwamnyeto ambao unaweza kuwa endelevu kwa miaka ijayo na itaweza kushirikisha timu mbalimbali.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad