MWANAMUME mmoja (54) ambaye ni mfanyakazi wa ujenzi nchini Marekani amefariki dunia baada ya kula pipi zilizotengenezwa kwa pombe maarufu kama liquorice.
MwanaMume huyo alikula mfuko mmoja na nusu wa pipi hizo kila siku, kabla ya kupata mshtuko wa moyo na hakuwa ameonYesha dalili zozote za kuugua alipokuwa kwenye mgahawa.
Daktari wake alisema tindikali ya glycyrrhizic iliyopo kwenye pipi hizo ndiyo chanzo cha kifo chake na utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa glycyrrhizic ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa pipi hizo na inasababisha shinikizo la juu la damu, kiwango cha chini cha potasiamu, mabadiliko makubwa ya mapigo ya moyo yenye uwezo wa kusababisha kifo na kushindwa kwenda haja ndogo.
Mwanamume huyo kabla ya kufariki alibadilisha aina ya pipi anazokula kutoka aina ya pipi nyekundu hadi nyeusi zinazotengenezwa kwa pombe.