Afrika kupokea dozi milioni 220 za chanjo ya Covid-19


Majaribio ya chanjo kwa binadamu yamekuwa ikiendelea kufanywa Afrika itakayoidhinishwaImage caption: Majaribio ya chanjo kwa binadamu yamekuwa ikiendelea kufanywa Afrika itakayoidhinishwa

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema chanjo ya Covid-19 itakapoaidhinishwa, Afrika itapata karibu dozi milioni 220 za awali.

Sehemu ya kwanza ya chanjo hiyo itapewa wafanyakazi wa afya na makundi yaliohatarini, kwa mujibu wa meneja mkuu wa mradi huo katika WHO Afrika, Richard Mihigo.

Amesmea usambazaji wa chanjo hizo utategemea idadi ya watu katika kila nchi.

Bwana Mihigo amesema nchi zote 54 barani humo zimeonesha nia ya kutaka chanjo ya Covid-19.

Afrika ina zaidi ya wato bilioni 1.3.

Mpango wa chanjo duniani unaofahamika kama COVAX, inakusudia kusaidia kununua na kusambaza kwa usawa dozi bilioni mbili za chanjo zilizoidhinishwa ifikapo mwisho wa mwaka 2021.

Mpango huo una chanjo tisa ambazo zinafanyiwa majaribio duniani

Chanjo mbili kati ya hizo zinafanyiwa majaribio Afrika, kwa mujibu wa mkuu wa muungano wa ubunifu wa maandalizi dhidi ya majanga (CEPI) bwana Richard Hatchett.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad