Afrika yapoteza mabilioni ya madola kupitia uhamishaji haramu wa fedha



Uhamishaji haramu wa fedha unahusishwa na usafirishaji nje wa bidhaa za thamani kama vile dhahabuImage caption: Uhamishaji haramu wa fedha unahusishwa na usafirishaji nje wa bidhaa za thamani kama vile dhahabu

Afrika imepoteza dola bilioni 836 sawa na (£650bn) kupitia uhamishaji haramu wa fedha kutoka barani humo kwa miaka 15 hadi mwaka 2015, ripoti mpya ya Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa inakadiria.


Uhamishaji huo haramu wa fedha unahusishwa na usafirishaji nje wa bidha za thamani kama vile dhahabu, almasi na platini. Fedha zinazopatikana kwa njia ya ufisadi, wizi na kukwepa kulipa kodi.


“Uhamishaji haramu wa fedha unainyang’anya Afrika na watu wake mali hali inayotokana na uhujumu wa uchumi ambayo inafanya taasisi zake kutoaminika,” alisema Katibu Mkuu wa UNCTAD Mukhisa Kituyi.


Ripoti hiyo inaonya kwamba ingawa kiasi cha mtiririko huo wa fedha haramu ni mkubwa, takwimu zinaweza kupuuza changamoto na athari.


''Uhamishaji haramu wa fedha pamoja na ufisadi ni hali ambayo inazuia maendeleo katika nchi za Afrika kuwa kumaliza pesa za kigeni, kupunguza raslimali nza ndani, kukwamishabiashara za kuimarisha uchumi na kuzidisha umasikini na ukosefu wa usawa.'', aliongeza kusema Bw. Kituyi.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad