Saratani ya Matiti..Vijue Viashiria Muhimu Kuhusu Ugonjwa Huo....



Saratani ya Matiti ni ugonjwa maarufu sana katika kuwapata Wanawake japokuwa unaweza kutokea kwa Wanaume ila ni nadra sana ikilinganishwa na Wanawake

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), inakadiriwa kuwa vifo 42,260 (Wanawake 41,760 na Wanaume 500) vinatokea kwasababu ya Ugonjwa huo kila mwaka na 62% ya Wanawake wanafariki kutokana na kushindwa kupima afya zao mara kwa mara

Idadi kubwa ya Wanawake hawajui viashiria vya mwanzo vya Saratani ya Matiti na kwa mujibu wa gazeti la Independent, 42% wanajua ni mabadiliko gani ya kuangalia kwenye matiti yao, huku robo ya Wanawake wakidhani kiashiria pekee ni uvimbe

Wanawake wanashauriwa kukagua matiti yao kila baada ya mwaka na kuangalia viashiria vifuatavyo; Uvimbe, Badiliko la Umbo au Muundo wa titi, Kutokwa na vipele vidogo au Ngozi kukakamaa na Chuchu kutoa majimaji

Aidha, viashiria vingine ni Ngozi kutokurudi katika hali ya kawaida baada ya kubonyezwa/kugandamizwa, Maumivu ya mara kwa mara, Mabadiliko katika mguso wa Ngozi, Kuvimba maeneo ya kwapa na Mabadiliko katika muonekano wa Chuchu(Kuingia ndani au kuchomoza)

Inashauriwa unapoona dalili kama hizi, ni vizuri kumuona daktari atakayefanya uchunguzi zaidi na baadaye kukupeleka kwa bingwa wa magonjwa hayo kwa ushauri na tiba zaidi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad