Ashindwa Kujuzuia na Kuangua Kilio Akiomba kura za Udiwani



Mgombea Udiwani Kata ya Mumbaka Masasi mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Salumu Mwinyiheri katika hali isiyokuwa ya kawaida alikatisha hotuba yake ghafla na kuaungusha kilio mbele ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo.




Mwinyiheri alimwaga machozi kuomba wananchi wa kata hiyo kumchagua kwani anasikitishwa na changamoto zinazowakabili wananchi hao ikiwemo migogoro ya ardhi pamoja na umilishwaji wa ardhi kwenye maneo yao.


Hayo yametokea jana katika mkutano wa kampeni za chama hicho na kufarijiwa kwa kufutwa machozi na baadhi ya wananchi wa kata hiyo pamoja na viongozi wa CUF waliokuwepo katika mkutano huo huku wananchi hao wakimuhakikishia kumpa kura kwa vile wameguswa na yeye kulia mbele yao.


Awali akizungumza kabla ya kukatisha hotuba yake, Mwinyiheri alisema katika kata hiyo kuna changamoto nyingi ambazo kama angekapata fursa ya kuwa Diwani wa kata hiyo angezifanyia kazi ya kuzitatua kwa nguvu zote ili wananchi waweze kunufaika na mafanikio chanya ya serikali.




Mwinyiheri alisema amekuwa na masikitiko mkubwa ndani ya nafsi yake na anatamani kuona baadhi ya changamoto zinazowakabili wananchi wa kata hiyo siku moja zinatatuliwa kwa kumpata kiongozi ambaye pia atakuwa na uchungu wa kutatua changamoto hizo ikiwemo umilikishwaji stahiki wa ardhi na ujenzi wa soko la kisasa.


Alisema katika kata hiyo kumekuwa na changamoto kadhaa ambazo yeye kama anapata fursa ya kuchaguliwa kuwa diwani atalazimika kushughulikia changamoto hizo kwa kuishawishi halmasshauri kutatua changamoto hizo kwa haraka.


Mwinyiheri alisema moja ya changamoto ambayo atahakikisha lazima ifanyiwe utatuzi ni suala la ulasimishwaji wa ardhi ili kila mwananchi aweze kuwa na hati miliki ya eneo lake na kwamba hati hiyo imuwezeshe mwananchi hata kupata mikopo kwennye taasisi za fedha.


“Kilio nilichoangusha hapa leo nimejikuta nikilia tu lakini sababu kubwa ni kwamba ninatamani sana kuwa diwani wa kata hii ili niwasaidie wananchi hawa maana wanachangamoto nyingi ikiwemo maji, barabara, afya kwa akinamama wajawazito pamoja migogoro ya ardhi,”alisema Mwinyiheli




Alisema iwapo wananchi hao wakifanya changuo sahihi la kuchagua diwani anayetokana na chama cha CUF ikiwemo na mbunge basi hata maendeleo ndani ya kata hiyo yatakuwa kwa kasi baadhi ya changamoto zingine ambazo zitatekelezwa ni pamoja na changamoto ya wakulima katika mazao yao.


Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF) Hassani Chariche alisema kuwa CUF ni chama ambacho kimezamiria kwa dhati kuona wananchi wilayani Masasi wanakuwa na maendeleo hivyo wananchi wasisite kukipa ridhaa ya kukichagua.


Alisema ili maendeleo yaweze kupatikana kwa haraka ndani ya kata hiyo CUF ipiwe kipaumbele kwa kuchaguliwa wagombea wake kuanzia ngazi ya kata, wabunge na raisi hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi oktoba 28 katika vituo vya kupiga kura ili kuwateua vigongozi hao wa CUF.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad