Azam Yapata Dawa Ya Kuzipiku Simba, Yanga


TIMU ya Azam FC imejinadi kuwa tayari imeshapata dawa ya mechi za mikoani ili kwenda sambamba na Simba na Yanga kwenye Ligi Kuu Bara kufuatia msimu uliopita kutofanya vema.



Azam wamesema msimu uliopita walipoteza mechi nyingi mkoani, hivyo wameamua kubadili mfumo wa mazoezi ili kuendana na hali ya viwanja vya mikoani ambavyo vingi vinaelezwa havina ubora.



Timu hiyo katika msimu uliopita ndani ya Ligi Kuu Bara, ilimaliza nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa, Simba na Yanga.



Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Tathimini iliyofanyika katika ripoti ya msimu uliopita jambo la msingi ambalo limeonekana ni utumiaji wa uwanja.



“Awali mazoezi yalikuwa yakifanyika sana kwenye uwanja wa nyasi badia jambo ambalo limetugharimu pindi timu inapokwenda kucheza mechi za mikoani katika viwanja vya kawaida.



“Hivyo kwa sasa Kocha Aristica Cioaba na benchi la ufundi wameamua wachezaji watafanyia mazoezi katika viwanja vyote viwili ili kuzoea mazingira kuhakikisha zinapokuja mechi za mikoani haziwapi tabu.



“Tunaamini tukifanya hivi timu itapata matokeo mazuri katika mechi za mikoani ambazo msimu uliopita zilitusumbua na kujikuta tukipoteza mechi nyingi.”Azam FC ina viwanja viwili vya mazoezi vilivyopo Chamazi jijini Dar. Kimoja ni cha nyasi bandia na kingine cha nyasi asili ambacho pia hukitumia kwa mechi za ligi na michuano mingine
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad