Mwanamke mmoja amewaaacha wengi midomo wazi baada ya kusimulia jinsi baba yake mzazi amekuwa akimnyanyasa na kufanya ngono naye tangu alipokuwa na miaka 13 baada ya mama yake mzazi kuaga dunia.
Huku akieleza masaibu ambayo amekumbana nayo alikuwa na haya ya kusema.
“Baba yangu amekuwa akininyanyasa kijinsia tangu nilipokuwa na miaka 13, kwa sasa niko na miaka 20 ninaishi kwa nyumba moja na baba yangu, sikwenda katika shule ya upili baada ya kufanya mtihani wa darasa la nane nina ndugu mmoja tu.” Alieleza mwanamke huyo.
Huku akieleza masaibu ambayo baba yake alifanya kwa ndoa yake baada ya kuolewa akiwa na miaka kumi na saba, alisema kuwa baba yake alimtishia mumewe ili waachane na kumaliza ndoa yao.
Mwanamke huyo wa kutoka Webuye alisema haya,
“Unyanyasaji huo ulianza wakati mama yangu aliaga dunia, tulienda mpaka kwa chifu lakini baba yangu alikataa kila kitu, chifu naye aliniambia sina ushahidi wa madai hayo
Pia nilitoroka nyumbani na kuingia katika ndoa nikiwa na miaka 17, ili nitoke tu nyumbani baba yangu alipigi mume wangu na kumtishia baba yangu aliharibu ndoa yangu
Nimejaribu kuwaambia hata majirani lakini hamna mmoja wao ananisaidia, pia amenichapa sana.” Alisimulia.