Charles “Chuck” Feeney ni bilionea ambaye alikuwa na ndoto za kumaliza mali yake yote akiwa hai, kwa kutoa fedha zake zote kwa mashirika ya hisani.
Mfanyabiashara huyo wa Marekani mwenye umri wa miaka 89 , hatimaye amefikia lengo lake siku chache ziliopita alipotoa dola, milioni 8,000 kusimamia miradi ya hisani duniani.
Hivi sasa hana nyumba wala gari na ni maarufu kwa kuvalia saa ilionunuliwa kwa dola 15 pekee.
”Nilikuwa na wazo ambalo halikuondoka katika fikra zangu, kwamba unapaswa kutumia mali yako kuwasaidia watu”, alisema mfanyabiashara huyo. Na kwa kipindi kirefu alichangisha fedha bila kujulikana.
Wakati mwandishi Gerardo Lissardy, kutoka BBC Mundo alipomuuliza 2017 kwanini alikuwa akifanya kuwa siri, alijibu, ”kwa sababu hakuna haja ya kuelezea watu kwanini unafanya hivyo”.
Kulingana na Conor O’Clery, aliyeandika kitabu kuhusu Feeney, anasema kwamba mtu huyo alipatiwa msukumo na kitabu cha ‘Mali’, kikijulikana, ‘The Gospel of Wealth’, kilichoandikwa na Andrew Carnegie.
Mishororo kama ”Kufa tajiri ni kufa kwa aibu”, iliwacha kovu katika fikra za Feeney. Alisafiri kote duniani kwa siri, akitafuta njia za kukamilisha kazi yake ndio maana aliitwa jina la Utani James Bond wa hisani.
Charles F. Feeney alizaliwa mjini Elizabeth, New Jersey mwaka 1931. Mama yake alifanya kazi kama nesi katika hospitali huku baba yake akiwa wakala wa bima.
Akiwa kijana mdogo alionesha uwezo wake wa kufanya biashara.
Aliuza kadi za krisimamsi mlango hadi mlango akiwa na umri wa miaka 10. Akiwa kijana alisajiliwa katika jeshi na kushiriki katika vita vya Korea.Chuck Feeney
Alitumia fursa ya mpango wa elimu wa Marekani kwa wakongwe na kuwa mtu wa kwanza wa familia yake kujiunga na chuo cha masomo.
Baada ya kuhitimu katika chuo kikuu cha Cornell University mjini New York , alianza biashara yake akiuza bidhaa kwa wanajeshi wa Marekani waliopo katika kambi barani Ulaya.
Biashara hiyo ilipiga hatua na kuwa maduka yasiotoza ushuru DFS kampuni ya mauzo isiotoza ushuru alioanzisha kwa pamoja na Robert Miller 1960.Chuck Feeney
”Sikufanya hivyo ili kuthibitisa chochote: Tajiri huyo aliyechangisha dola bilioni nane na kuwachwa na bila kitu.
”Watu wanapaswa kuchukua jukumu kutumia baadhi ya mali yao kuimarisha maisha ya wanadamu wenzao, la sivyo watajenga matatizo makubwa katika vizazi vya siku za baadaye”.
Kwa sasa anaishi katika nyumba ya vyumba viwili katika mji wa San Fransisco na mkewe Helga.
Mwaka 1982 alianzisha wakfu wa Atlantic Philanthropies Foundation , shirika la kimataifa kusambaza mali kwa miradi ya hisani duniani.
Katika kipindi cha miaka 15 ya kwanza, Feeney kisiri alichangisha fedha, na kumfanya kuitwa James Bond wa hisani, hadi alipojitokeza 1997.The Lanyon Building at Queen's University Belfast
Ufadhili umetajwa kubadili maisha ya wengi
Tangu alipoanzisha wakfu wa Atlatntic Phillanthropies, ametoa karibia dola bilioni nane kama misaada.
Wakfu huo umetangaza kwamba utasitisha operesheni zake siku ya mwisho ya mwaka wa 2020 baada ya lengo la Feeny kuafikiwa,
Filosofia yake ya kutoa wakati unapoishi imewapatia msukumo mabilionea wengi, ikiwemo mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates na mwekezaji Warren Buffet.
Feeney hajulikani sana kama matajiri wengine kwasababu ya kutoa michango yake kisiri katika kipindi cha kwanza cha miaka 15 cha kazi yake