Bobi Wine ashitakiwa kwa kuhadaa kuhusu umri wake



Bobi Wine anasema madai hayo ni jaribio lingine la kuhujumu upinzaniImage caption: Bobi Wine anasema madai hayo ni jaribio lingine la kuhujumu upinzani

Mahakama nchini Uganda imemtaka mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, kufika mbele yake kujibu tuhuma za kutoa taarifa za uwongo kuhusu umri wake kwa Tume ya Uchaguzi.

Bobi Wine anatakiwa kufika mbele ya mahakama hiyo kabla ya Septemba 16 kujibu kesi iliyowasilishwa na wakili, Male Mabirizi.

Katika ombi lake la Agosti 3, bwana Mabirizi anadai vyeti vya masomo vya Bobi Wine vinaonesha alizaliwa tarehe 12 Februari 1980, tofauti na tarehe iliyonakiliwa katika pasipoti yake na pamoja na fomo aliyowasilisha kwa tume ya uchaguzi mwaka 2017 wakati alipoteuliwa kugombea kiti cha ubunge.

Pasipoti ya Bobi Wine inaonenesha kuwa alizaliwa Februari 12,1982.

Pia anakabiliwa na mashitaka ya "kupata usajili kwa njia ya udanganyifu" katika mahakama hiyo.

Mjadala kuhusu miaka ya mtia nia huyo wa kugombea kiti cha urais na uhalisia wa vyeti vyake vya elimu umezua gumzo katika mitandao ya kijamiikwa majuma kadhaa.

Bobi Wine aliweka ujumbe katikamtandao wa Facebook Siku ya Jumatatu, akisema kesi ya hivi punde dhidi yake ni sehemu ya muendelezo wa njama ya serikali kuhujumu upinzani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad