MADUKA matatu yaliyopo maeneo ya Sinza-Mapambano jijini Dar es Salaam karibu na Ofisi za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) yameteketea kwa moto leo Jumatatu, Septemba 7, 2020, asubuhi, majira ya saa tano.
Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na taarifa zaidi juu ya uharibifu wa mali zilizoteketea bado hazijatolewa.