Bunge la Somalia, limemuidhinisha Mohamed Hussein Roble kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo baada ya wabunge wote 215 waliohudhuria kikao cha bunge, leo, Septemba 23, 2020 kumpigia kura ya ndiyo.
Roble anachukua nafasi ya Hassan Ali Khaire ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Mohamed Abdullahi Mohamed Julai, 2020.
Mwanasiasa huyo chipukizi, alipendekezwa na rais siku tano zilizopita ambazo kilichokuwa kikisubiriwa ilikuwa ni bunge linaloongozwa na Spika Mohamed Mursal kumuidhinisha.