CCM Yatangaza Mikakati ya ushindi ya chama hicho.




Katibu Mwenezi na Itikadi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema Kampeni kwa ujumla zinaendelea vizuri na washamewafikia Watanzania wengi na wanawaelewa. 


Polepole ameongeza kuwa CCM imefanya tafiti za Kisayansi na kugundua kama kura zikipigwa sasa hivi, Mgombea wao wa nafasi ya Urais, Dkt. Magufuli ataibuka na ushindi mnono wa asilimia 85, hivyo kwa sasa wanajazia tu kura. 


Amesema hayo leo Ijumaa, Septemba 11, 2020 wakati akizungumza na wanahabari mkoani Geita na kutoa tathmini ya kampeni za CCM kwa siku 12 walizofanya na kutoa mwongozo kwa awamu ya pili ya kampeni za chama hicho. 


“Kampeni kwa ujumla inakwenda vizuri sana, tumewafikia Watanzania na wametuelea mno, tumefanya tafiti za kisayansi kwa sababu tupo makini, kama kura zikipigwa sasa hizi Mheshimiwa Magufuli anaibuka na ushindi mnono wa asilimia 85, sasa hivi tunajazia tu kura.


“Kwa mujibu wa kitengo chetu cha taarifa cha chama chetu, kule mambo yameharibika, tumeona mmoja wa wagombea amekimbia, amechomoka mapema sana usiku wa kuamkia leo, hayupo nchini hapa.- Amesema. 


Kuhusu mikakati ya ushindi ya chama hicho, Polepole amesema, katika uchaguzi huu CCM imeboresha kampeni zake kwa kugawanya makada wake waandamizi katika maeneo tofauti tofauti kwa ajili ya kushambulia kila kona.


Akitangaza safu hiyo ya ushindi, Polepole amesema safu ya kwanza ni ya Mgombea Urais wa Tanzania, John Magufuli, ya pili ikiwa ni ya Mama Samia Suluhu Hassan, mgombea mwenza wakati ya tatu ikiwa ni ya Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu.


Safu ya nne inaongozwa na Kikwete huku safu ya tano ikiongozwa na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda, akishirikiana na Spika wa Tanzania Job Ndugai.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad