Chidi Benz na filamu ya maisha yake



Kama ulitazama show ya Friday Night Live ya East Africa TV siku ya Septemba 25, 2020 najua utakuwa umefurahia au kuburudika kwa kile kilichotokea na Suprise ambazo zimefanyika wakati show hiyo ikiendelea.


Walipita wasanii wengi kama Kayumba, Jumanne Iddi, Rasco Sembo, Barakah The Prince, Country Boy na Chidi Benz.

Kuhusu Chidi Benz ametoa taarifa maalumu baada ya mpenzi wake kumshauri kuachia filamu ambayo itakuwa inaonyesha uhalisia wa maisha yake na yote ambayo amewahi kuyapitia.

Akizungumiza hilo Chidi  Benz amesema "Jana mpenzi wangu ameniambia hivyo na tulikuwa tunajadiliana kuhusu hilo, akaniambia nikifanya filamu yangu itakuwa poa sana ila inatakiwa kupangwa vizuri ila sio kukurupuka maana itakuwa kama bangi".

Kingine Chidi Benz amesema watu wanatakiwa wawaheshimu sana baba zao hata kama waliwahi kuwakosea pia hakuna sababu yoyote kwa mtoto wa kiume kugombana na baba yake.


Zaidi mtazame hapa chini akifunguka kuhusiana na hayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad