Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta amejiunga na club ya Fenerbahce ya Uturuki akitokea Aston Villa ya England, bado Fenerbahce haijaweka wazi kama wamemsajili kwa mkopo wa msimu mzima 2020/21 kama inavyoripotiwa au ni uhamisho kamili.
Fenerbahce wamempa jezi namba 12 Mbwana Samatta ambaye anaenda kuongeza nguvu katika kikosi hicho, club hiyo imewahi kumuwania mara kadhaa hata kabla ya kwenda Aston Villa lakini ndoto ya Samatta ilikuwa ni kucheza EPL
Samatta anaondoka Aston Villa baada ya nafasi yake ya kucheza kuwafinyu sababu Aston Villa wamesajili wachezaji wengine wawili wa nafasi ya ushambuliaji Watkins na Traore, pamoja na Samatta nafasi hiyo ingekuwa na jumla ya wachezaji wanne.