Utawala wa rais Donald Trump wa Marekani utatangaza leo kuwa utaondoa wanajeshi zaidi kutoka Iraq, wakati rais huyo akijaribu kutimiza ahadi yake ya kampeni ya kuiondoa nchi hiyo kutoka vita visivyoisha.
Afisa mwandamizi wa utawala huo alijadili hatua hiyo ya kupunguza wanajeshi na waandishi habari katika ndege ya rais ya Air Force one, jana usiku, kwa masharti ya kutotajwa jina.
Afisa huyo alisema utawala wa rais Trump pia unaangalia kutangaza kuondolewa kwa wanajeshi zaidi kutoka Afghanistan katika siku zijazo.
Tangazo hilo lililopangwa kutolewa linakuja wakati rais Trump akijaribu kuelezea kuwa ametimiza ahadi zake alizotoa miaka minne iliyopita wakati akijaribu kupata muhula wa pili madarakani. Kuna zaidi ya wanajeshi 5,000 nchini Iraq hivi sasa.